Looking for more resources for supporting parents during COVID-19? Visit the Start Talking Now Facebook page.

Wazazi na Walezi

You are here

Home » Wazazi na Walezi

Bonyeza hapa uone tovuti nzima katika Kiswahili 

Ukurasa huu una maelezo kuhusu:

Wewe ndiye mshawishi mkuu zaidi katika maamuzi ambayo kijana wako atafanya kuhusu dawa za kulevya.

Zaidi ya marafiki zake. Zaidi ya watu mashuhuri. Ndiyo maana ni muhimu kwa vijana kusikia maoni yako kuhusu kuepuka kutumia bangi, pombe au dawa nyingine za kulevya, na wao kujifunza kufanya maamuzi bora, ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu bora za kukabiliana na changamoto maishani.

Kuzungumza na kijana wako kuhusu mada hizi kunaweza kuwa jambo gumu, lakini utafiti unaonyesha kuwa ni mojawapo ya mambo muhimu zaidi unayoweza kufanya ili kumwonyesha kuwa unamjali, kuweka viwango vya matarajio, na kumsaidia kudumisha usalama na afya yake. Mazungumzo yanaweza kuwa ya kawaida na mafupi ambayo unafanya unapoendelea na shughuli na kijana wako. Hii hapa orodha ya majibu ya maswali ambayo mtoto wako anaweza kuuliza kuhusu pombe na bangi, ili kukusaidia kujiandaa kufanya mazungumzo haya. Watu wote hawafanani, kwa hivyo kumbuka kubadilisha majibu yako kulingana na maoni na uzoefu wako mwenyewe. Kufanya mazungumzo ya kibinafsi na ya dhati kutakuwa na matokeo bora zaidi.

Hizi hapa nyenzo za ziada za kukusaidia kuzungumza na vijana wako:

Vidokezo kwa wazazi na walezi.

Fanya shughuli na kijana wako, fanya mazungumzo ya mara kwa mara, na mfanye shughuli za kuburudisha pamoja!

Unaweza kumsaidia kijana wako kuepuka bangi, pombe au dawa zingine mnapochangamana, kuweka masharti na kufuatilia.

Jenga mahusiano ya karibu.

Vijana wana uwezekano mdogo zaidi wa kutumia pombe au bangi au dawa zingine ikiwa wazazi na/au walezi wao wanahusika katika maisha yao na wanapohisi kuwa wanahusiana kwa karibu. Ili kuongeza uhusiano wa kifamilia:

 • Mpe mtoto wako angalau dakika 15 za mahusiano ya karibu kila siku.
 • Fanyeni mambo ya kuburudisha pamoja.
 • Mpongeze kwa kuhusu chaguo bora kwa afya ambazo mtoto wako anazofanya.
 • Kuleni pamoja.

Weka masharti wazi.

Weka sheria wazi mwanzoni, dumisha uthabiti na uzungumze kuhusu miongozo mara kwa mara. Ili kuweka mipaka:

 • Fanya mazungumzo ya mara kwa mara kuhusu matarajio yako.
 • Tumia nidhamu ya haki na thabiti wakati ambapo mtoto amevunja kanuni zako.
 • Wasaidie watoto wako kuwa na uhusiano mzuri na marafiki.
 • Msaidie mtoto wako ajizoeze kukataa dawa za kulevya.

Fuatilia mahusiano.

Fahamu kila mara jambo ambalo kijana analifanya, anakoenda na anakaa na nani. Msaidie kupanga shughuli salama na za kufurahisha. Kumbuka kuuliza maswali haya matano:

 • Unaenda wapi?
 • Utakuwa ukifanya nini?
 • Utakuwa na nani?
 • Utarudi nyumbani lini?
 • Je, kutakuwa na pombe, bangi au dawa nyinginezo za kulevya?

Kuna hatari gani za utumiaji pombe, bangi na dawa zingine za kulevya?

Utumiaji wa mapema wa pombe, bangi, na dawa nyinginezo huwaweka vijana katika hatari kubwa ya uraibu na matatizo mengine ya afya, kufeli shuleni, na chaguo ndogo za kazi zinazoathiriwa na kukamatwa na ukosefu wa elimu. Bangi, pombe na matumizi mengine ya dawa za kulevya:

 • Yanaweza kusababisha madhara ya ubongo kwa kijana wanaokomaa. Pombe, bangi na dawa zingine zinaweza kudhoofisha sehemu za ubongo zinazodhibiti uratibu wa mwenzo, udhibiti wa msukumo, kumbukumbu, kujifunza na uamuzi. Ubongo wa vijana huathirika zaidi kwa sababu bado unakua.
 • Ulevi unaweza kusababisha uraibu. Watoto wanaokunywa pombe kabla ya umri wa miaka 15 wana uwezekano mara nne zaidi wa kutatizwa sana na ulevi wakiwa watu wazima, na wale wanaoanza kutumia bangi kabla ya umri wa miaka 18 wana uwezekano mara nne hadi saba wa kupata tatizo la kutumia bangi kuliko wale wanaoitumia baadaye maishani.
 • Ulevi unahusishwa na sababu tatu kuu za vifo vya vijana: Ajali (ikiwa ni pamoja na vifo vya barabarani na kuzama majini), mauaji na kujiua.

Pata ukweli kuhusu hatari za matumizi ya dawa za kulevya kwa watu wa umri mdogo.

Kuza tabia njema kwa pamoja.

Msaidie kijana wako kukuza tabia njema, kuweka malengo na kujizoeza njia bora za kukabiliana nayo.

 • Kuweka malengo: Kuweka malengo huwapa watu hisia ya kuwa na kusudi na huwasaidia kuamini kuwa watakuwa na maisha bora ya siku zijazo. Wakati wa sasa unaweza kuwa wenye changamoto, lakini ni rahisi kukabiliana nao mtu akiwa na matumaini kuhusu fursa za siku zijazo. Zungumza na kijana wako kuhusu mambo anayotaka kufanya katika siku zijazo na umsaidie kuweka mipango.
 • Kudumisha tabia njema: Kula vizuri, kulala vya kutosha na kufanya mazoezi huboresha afya na hisia njema. Weka mpango (kama vile nyakati za kula), ambayo huwezesha mtindo bora, na izungumze na kijana wako kuhusu umuhimu wa tabia njema. Kwa pamoja, panga mikakati ya kuimarisha na kudumisha tabia njema.
 • Kukuza ujuzi wa kukabiliana na hali ngumu: Ni muhimu kwa vijana kutambua shughuli zinazowasaidia kuhisi vizuri wanapokabiliwa na mfadhaiko au wasiwasi. Kwa kushirikiana na kijana wako, tafuta njia za kujumuisha shughuli hizo maishani mwake — iwe ni kucheza mpira kwenye uwanja wa nyuma ya nyumba baada ya chakula cha jioni, kutembea mtaani, vipindi vya sanaa vya kila siku au kuhesabu tu hadi 10 na kupumua kwa kina akihisi kuwa mambo yanakwenda kombo.

Pata usaidizi.

Ni sawa kuomba usaidizi kwa niamba yako na ya kijana wako! Nyenzo zote zilizo hapa chini zinatoa TSR 711 na huduma za ufikiaji wa lugha.

 • Teen Link ni huduma ya simu ya usaidizi usiolipishwa na wa siri ambayo vijana wanaweza kutumia kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi au kupiga gumzo na vijana waliofunzwa kuanzia 6 p.m. hadi 10 p.m. PT. Mtoto wako anaweza kuzungumza naye kuhusu chochote anachowazia. Mhimize mtoto wako kupiga simu, kutuma SMS au kupiga gumzo kwa 1-866-TEENLINK (833-6546). Watu wazima pia wanaweza kupigia simu Teen Link ili kuzungumza na daktari aliyebobea katika huduma ya kuzuia ulevi. Tembelea www.teenlink.org upate maelezo zaidi.
 • Washington Recovery Help Line ni huduma ya usaidizi wa simu wa saa 24 ya siri na isiyowatambulisha watu, ambayo hutoa usaidizi kwa wale wanaokabiliana na matatizo ya matumizi ya dawa na changamoto za afya ya akili. Piga simu 1-866-789-1511 au utembelee WARecoveryHelpLine.org upate maelezo zaidi.
 • Washington Listens hutoa usaidizi kwa watu wanaokabiliwa na hisia za huzuni, wasiwasi au mfadhaiko. Wahudumu wake wanapatikana Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 9 a.m. hadi 9 p.m. PT na wikendi kutoka 9 a.m. hadi 6 p.m. PT. Tembelea tovuti ya Washington Listens upate maelezo zaidi.